Chaneli ya Utalii (Tanzania Safari Channel) ilizinduliwa rasmi na Mheshimiwa Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tarehe 15/12/2018. Lengo la kuanzisha Chaneli hii ni kukuza utalii wa ndani na nje na halikadhalika kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa uhifadhi. Maudhui ya Chaneli hii yanalenga kuangazia maeneo ya uhifadhi kama vile: Wanyama wa porini, Viumbe wa Baharini, Misitu, Fukwe, Miamba na Majabari, Utamaduni, Malikale, Michezo, Kumbi za Mikutano na mengineyo. Madhumuni ya Chaneli hii ni pamoja na: i. Kuwawezesha Watanzania kuona na kubaini vivutio mbalimbali vilivyoko katika maeneo yote nchini; ii. Kuwahamasisha wananchi wajenge utamaduni wa kutembelea maeneo yenye vivutio nchini; iii. Kutangaza duniani vivutio vya utalii vilivyopo Tanzania ili kuongeza idadi ya watalii kutoka nje ya Nchi; iv. Kuieleza na kuikumbusha Dunia kwamba Mlima Kilimanjaro, Hifadhi ya Serengeti, Ngorongoro na hata Zanzibar vipo Tanzania; v. Kuhamasisha wananchi kutunza, kuenzi na kudumisha tamaduni za asili; vi. Kuangazia na kuibua fursa mbalimbali zilizopo kwenye mnyororo wa biashara katika Sekta ya Utalii; na vii. Kuyaenzi maneno ya Baba wa Taifa Mwalimu, Julius Kambarage Nyerere, aliyoyatoa mwaka 1961, kwamba “sisi sote tuna jukumu kubwa la kulinda na kuhifadhi vivutio vya utalii kwa manufaa ya vizazi vilivyopo na vijavyo”.
APKFab.com和該應用的下載連結是100%安全的。APKFab.com上列出的所有應用下載連結均來自Google Play Store或由用戶提交。對於來自Google Play商店的應用,APKFab.com不會對其進行任何形式的修改。對於用戶提交的應用,APKFab.com會在網站上發佈之前驗證其APK簽名的安全性。