Kwa Jina La Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu Kusoma na kuandika kwa khati za Kiarabu ni jambo jepesi. Wazee wetu wa Kiswahili waliokuwa visiwani Unguja, Pemba, Mombasa, Lamu na Mafia na waliokuwa mrima na mwambao wote wa Afrika Mashariki na katika miji ya asli ya Bara kama Tabora na Kigoma, karibu wote walikuwa wakijua kusoma Kuruani na wakijua kuandika na kusoma Kiswahili wakitumia harufi za Kiarabu kabla ya kufika mkoloni na kuleta Jifunze Kusoma Kiarabu hizi harufi za Kizungu zinazotumiwa sana hivi sasa. Walipofika Wazungu wa mwanzo nchi ya Uganda waliwakuta watawala wenyeji wakiandikiana wao kwa wao kwa maandishi ya Kiarabu. Yamkini wakitumia Kiarabu au Kiswahili kwa maandishi ya Kiarabu. Lugha ya Kiarabu ni moja katika lugha kubwa za dunia. Ni lugha iliyoandikiwa vitabu vingi sana na ilimu za kila aina, lakini khasa ni lugha ya Waislamu wote katika dini yao, na lugha ya sehemu kubwa kabisa katika Bara la Afrika. Harufi za Kiarabu zinafuatana zaidi na matamshi fasihi ya lugha ya Kiswahili. Kwa hivyo mwenye kujua kusoma na k'uandika kwa harufi ya Kiarabu, ataweza kusoma Kuruani kwa namna ilivyoteremka kwa Mtume S.A.W., na pia kitatengenea Kiswahili chake kiwe fasihi zaidi. Yafaa kabla ya kuanza kusoma tujue kuwa Kiarabu kinaanza kulia kuendea kushoto, kinyume na maandishi ya Kizungu. Tena harufi zisizotamkwa bali zasaidia kutamka, vokali, haziitwi harufi, bali huitwa irabu kama A,I,U zinapokuja baada ya Konsonanti. Hizo konsonanti, kama B, T, R, H, M, N, D, Z, K n.k. ndizo zinazoitwa harufi.
APKFab.com和該應用的下載連結是100%安全的。APKFab.com上列出的所有應用下載連結均來自Google Play Store或由用戶提交。對於來自Google Play商店的應用,APKFab.com不會對其進行任何形式的修改。對於用戶提交的應用,APKFab.com會在網站上發佈之前驗證其APK簽名的安全性。