首頁 編輯推薦 測評 資訊 相似應用 TopTens 預註冊 限時促銷 熱門遊戲 熱門應用 分類 APK Downloader APK Upload Chrome外掛程式 APKFab 客戶端 搜索應用
選擇語言

Herufi na Akili – Akili and Me

8.7 82

v1.0.0 by Ubongo

通過APKFab客戶端下載
安全快速安裝 - 無區域限制

關於 Herufi na Akili – Akili and Me

Herufi na Akili – Akili and Me(包名:co.ubongo.herufi.na.akili)開發者是Ubongo,Herufi na Akili – Akili and Me的最新版本1.0.0更新時間為2017年01月05日。Herufi na Akili – Akili and Me的分類是教育。您可以查看Herufi na Akili – Akili and Me的開發者下的所有應用並找到Herufi na Akili – Akili and Me在安卓上的2個相似應用。目前這個應用免費。該應用可以從APKFab或Google Play下載到Android 2.3.2+。APKFab.com的所有APK/XAPK文檔都是原始文檔並且100%安全下載的資源。
Sasa shule zimeanza rasmi. Je, wayajua maendeleo ya mwanao? Umemwandaa kufanya vizuri mwaka huu?
App yetu ya “Herufi na Akili” itampatia mwanao msingi imara wa Elimu!
App hii ni tafsiri ya Kiswahili ya #Akili's Alphabet: Game #1 ya Elimu Tanzania yenye mashabiki wengi, liyopakuliwa zaidi ya mara 10,000 kwenye Play Store!
“Herufi na Akili” inamwandaa mtoto wako kwa ajili ya kwenda SHULE. App hii hutumia michezo na nyimbo kufundisha mwanao jinsi ya kutamka herufi na kumfunza maneno mapya!
Mtoto wako atafurahia ELIMU na app hii ya BURE inayoletwa kwako na waandaaji wa katuni murua ya elimu-burudani ya “Akili and Me.”!
Mwanao atajifunza na Happy Hippo, Bush Baby na Little Lion, akiimba na kusikiliza nyimbo za herufi azipendazo kutoka kwenye kipindi cha "Akili and Me."
Hebu mwone anavyocheza kwa raha, akifurahi na marafiki huku akisikiliza HERUFI zinavyotamkwa na kuzifananisha kwenye simu!
Ubongo, ambao pia ni waandaaji wa katuni nyingine maarufu ya “Ubongo Kids”, wameitengeneza app hii kwa lengo hasa la kumwezesha mtoto wako:
FAIDA
- Atambue sauti za herufi.
- Afananishe herufi.
- Ajifunze kwa uwezo na kasi yake mwenyewe.
- Acheze kwa uhuru.
- Apende kujifunza.
VILIVYOMO
- Jifunze zaidi ya maneno 80 mapya.
- Cheza kwenye mazingira salama kwa ajili ya mtoto.
- Imebuniwa kwa ajili ya watoto wa miaka 3, 4, 5 na 6.
- Haina maksi wala daraja, hivyo mtoto atajifunza bila hofu.
- Ni BURE kabisa. Hakuna gharama zozote.
- Inafanya kazi BILA MTANDAO.
Ubunifu wa “Herufi na Akili” ni kwa ajili hasa ya watoto, hivyo mwanao ataielewa app hii bila shida na kuanza kuitumia mara moja.
Mwonyeshe jinsi ya kupanga na kuoanisha herufi mara moja au mbili tu, kisha tazama jinsi anavyocheza mwenyewe kwa uhuru kabisa na kwa raha zake!
Wangoja nini? Ipakue sasa BURE!
KIINGEREZA - AKILI'S ALPHABET
Ahsante kwa kupakua Herufi na Akili. Tumekuandalia pia tafsiri ya app hii inayoitwa "Akili's Alphabet" inayomfundisha mwanao sauti za herufi na maneno mapya kwa lugha ya Kiingereza.
"Akili's Alphabet" itamwezesha mtoto wako ajifunze lugha ya pili, huku akicheza na kusikiliza nyimbo alizozizoea kutoka kwenye kipindi cha "Akili and Me." Tafuta tu "Akili's Alphabet" hapa Google Play, na utaipata mara moja.
KUHUSU “AKILI AND ME”
“Akili and Me” ni katuni murua ya elimu na burudani inayoandaliwa na Ubongo, watengenezaji wa “Ubongo Kids” na programu nyingine nyingi za kujifunza zilizoundwa mahususi kwa ajili ya watoto wa Afrika.
Karibu Lala Land, ulimwengu wa maajabu, ambapo utajifunza na kucheza na Akili! Imba namba! Cheza herufi! Cheka, chora, na jifunze Kiingereza na Kiswahili na Akili.
Njoo ufurahi na Little Lion, Happy Hippo na Bush Baby kila Jumamosi na Jumapili saa 3 asubuhi kupitia TBC1 (Tanzania), na Jumamosi pekee saa 3 asubuhi kupitia Citizen TV (Kenya).
KUHUSU UBONGO
Ubongo ni kampuni ya kijamii ya Tanzania inayoandaa vipindi na katuni mahususi za elimu na burudani kwa ajili ya watoto wa Afrika, ikitumia teknolojia za kidijitali kama redio, simu, televisheni na vitabu vya mtandaoni kuwafikia popote pale walipo.
Mkakati wetu ni kuwafurahisha wana wa Afrika, tukiwafunza ili wapende kujifunza zaidi kwa uwezo na nafasi yao, wakitumia teknolojia walizo nazo. Njoo utazame vipindi maarufu vya “Ubongo Kids” na “Akili and Me” vinavyofikia zaidi ya nyumba milioni 5.1 barani Afrika.
ONGEA NASI
Kama una maswali, maoni, ushauri ama unahitaji msaada wowote, tafadhali zungumza nasi kupitia info@ubongo.co.tz. Twafurahi sana unapotupa maoni yako.
查看更多
Herufi na Akili – Akili and Me 資訊

歷史版本

更多

Herufi na Akili – Akili and Me 1.0.0 APK 2017年01月14日 36.61 MB 下載

Requires Android: Android 2.3.2+

Architecture: armeabi-v7a, x86

Screen DPI: 120-640dpi

SHA1: 21144ebb347d4c9cf893c0469261361ae5d43f70

Size: 36.61 MB

更多資訊

更新日期:

最新版本:

1.0.0

請求更新:

提交最新版本

系統要求:

Android 2.3.2+

安全下載

APKFab.com和該應用的下載連結是100%安全的。APKFab.com上列出的所有應用下載連結均來自Google Play Store或由用戶提交。對於來自Google Play商店的應用,APKFab.com不會對其進行任何形式的修改。對於用戶提交的應用,APKFab.com會在網站上發佈之前驗證其APK簽名的安全性。

分享
如果覺得這個頁面有用,可以分享給你朋友!